Mkulima wa mbogamboga shamba la
Zigi Kange Tanga, Helena Bahati, akimwagilia maji mboga aina ya Spinach,
wakulima wa kilimo hicho wamekuwa wakilalamika kipato kidogo wanachopata baada
ya kukosa soko la uhakika la kuuzia mbogamboga zao na kufuatwa na wachuuzi
shambani na kuwauzia kwa bei ya hasara.
Mkulima wa mbogamboga shamba la Zigi Kange Tanga, Helena Bahati, akivuna mboga aina ya Spinach katika shamba lake kupeleka katika masokoni . wakulimahao wamekuwa wakiendesha kilimo chao kwa hasara baada ya kukosa soko la uhakika la kuuzia mbogamboga zao.
Mkulima wa mbogamboga shamba la Zigi Kange Tanga, Helena Bahati, akifunga mboga zake kupeleka sokoni ambako soko lake halina uhakika, wakulima wa mashamba hayo wamekuwa wakilalamika kukosa soko la uhakika la kuuzia mboga zao na badala yake wachuuzi wamekuwa wakifika mashambani na kuwalangua kwa bei ya hasara, kifungu kimoja cha mboga Spinach kilikuwa kikiuzwa kwa shilingi 250 shambani.
Hali hii imekuwa kero na wakulima wengi kuiomba Serikali kuwajengea kiwanda cha kusindika matunda na mbogamboga ili kuweza kukiendeleza kilimo chao.
No comments:
Post a Comment