Magari yanayotumia nguvu za umeme yameanza kuuzwa nchini Kenya kwa mara ya kwanza. Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo.
"Watu
wengi wamekuwa wakiduwazwa na gari hili mitaani hapa jijini Nairobi, na
wengi wamependezwa nalo," anasema Francis Romano, msimamizi wa kampuni
Knights Energy, inayohamasisha watu watumie magari ya aina hiyo. Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo hii ikiwa
na maana kwamba hazitoi moshi au gesi zinazochangia ongezeko la joto
duniani kwa hivyo yanafaa mazingira.
Linaendeshwa kwa njia karibu sawa na gari la kawaida.
Hata
hivyo gari hilo lina uwezo wa kusafiri umbali wa takriban kilomita 90
hadi 135 kabla ya betri zake kuisha chaji, kasi yake ya juu zaidi ikiwa
kilomita 180 kwa saa. Upungufu mwingine ni ukosefu wa vituo vya kuchaji
gari hilo, na huenda ukakwama ukiwa katika maeneo ya mashambani ambapo
hamna nguvu za umeme ama pia vituo vya kuweka chaji. Hili limesababisha magari hayo kutumiwa Nairobi na viungani mwake pekee.
Hata
ingawa gharama ya ukarabati wa gari hilo ni ya chini mno, itakuwa
vigumu kwa watakaolinunua kupata vifaa mpya iwapo gari hilo litapata
hitilafu. Ya kwanza ina uwezo wa kuweka chaji kikamilifu kwa
muda wa saa nane, ya pili ina uwezo wa kuweka chaji kwa takriban saa
nne, huku ya tatu ikiwa na uwezo wa kuweka chaji kwa kati ya takriban
dakika 15 na saa mbili.
Bei ya gari hilo aina ya Nissan Leaf ni $10,000 (£7,600).
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment