WANAFUNZI W AKIUME UINGEREZA WATINGA SHULENI NA SKETI
Wavulana wavalia sketi shuleni Uingereza
Wavulana wanne katika shule moja nchini
Uingereza wamefika shuleni wakiwa wamevalia sketi kulalamikia hatua ya
mwalimu kuwaadhibu kwa kuvalia kaptura siku yenye joto kali zaidi nchini
humo.Wanafunzi hao wa darasa la mwaka wa tisa katika shule
yaLonghill eneo la Rottingdean, Sussex Mashariki, walikuwa miongoni mwa
wanafunzi 20 wavulana waliovalia kaptura za kuvaliwa wakati wa mazoezi
badala ya suruali ndefu.
Baadhi walifukuzwa shuleni Jumanne na
wengine kutengwa hadi siku iliyofuata. Waliokubali kuvua kaptura hizo na
kuvalia suruali ndefu hawakuadhibiwa.
Lakini badala ya kuvalia
sare kamili ya wakati wa masomo, kama walivyokuwa wameagizwa, wanafunzi
wanne walirejea shuleni Alhamisi wakiwa wamevalia sketi. Watatu waliambia wavue sketi hizo lakini wote kwa pamoja wakakataa na ndipo wakaruhusiwa kuendelea kukaa shuleni.
Mwalimu mkuu Kate Williams aliwaambia wanaweza kuvalia mavazi yoyote, mradi yawe ni sehemu ya sare iliyokubalika shuleni.
BBC
No comments:
Post a Comment