Watu wapewa likizo India kwa sababu ya filamu
Inahofiwa wengine huenda hata wangezima simu zao au kutofika kazini bila kueleza sababu.
Filamu hiyo kwa jina Kabali inaonyeshwa katika kumbi 12,000 za sinema leo.
Rajinikanth, ni mmoja wa waigizaji wanaolipwa pesa nyingi sana bara Asia na mmoja wa waigizaji mashuhuri zaidi kutoka India.
Hata kabla ya kuzinduliwa, filamu hiyo ya Kabali, ambayo inaangazia uhalifu wa magenge, imejizolea $30m (£20m) kupitia mauzo ya haki zake.
Itatolewa pia kwa lugha za Kitelugu, Kihindi na Kimalay.
Kampuni moja inasema imechukua hatua hiyo kuzuia watu kufika kwa wingi wakiomba likizo siku ya leo.
, mwenye umri wa miaka 65, ameigiza katika filamu zaidi ya 170, nyingi katika lugha ya Kitamil.
No comments:
Post a Comment