Mahakama kunusuru soka Hispania
Mahakama
moja nchini Hispania imepiga marufuku mgomo uliokuwa unaandaliwa na
muungano wa wanamichezo wa soka nchini humo ambao ulikuwa umepangwa kutekelezwa
mwishoni mwa wiki hii.
Mgomo huo ulianza kuhamasishwa wiki
iliyopita kufuatia hatua ya serikali ya nchi hiyo kutoa tamko la kurejea
upya haki ya urushaji matangazo ya mpira.Maamuzi ya mahakama hiyo yanatoa nafasi kwa pande zote mbili kuweka taratibu za namna ya kuutatua mzozo huo,ambao unatishia kuuzika mpira nchini humo na hata kuweka shaka ya kutooneshwa kwa mtanange baina ya timu mbili za Atletico Madrid na Barcelona.
Muungano huo wa wachezaji nchini Hispania, umesema kwamba serikali yao imejipanga kuweka mipango ya kisheria juu ya nini cha kufanya na kipi kisifanyike kuhakikisha kila klabu inalipa ushuru kuanzia vilabu vikubwa mpaka vya hadhi ya chini.
Ni halali yako kupata kile kinachonifikia na niko tayari kukutumia kupitia hapa hapa tangakumechablog, usiwe mbani nami
No comments:
Post a Comment