Kilichoendelea baada ya watu kumvamia mzee aliyedaiwa kujeruhi watu kwa bastola
Jana kulikuwa na stori kutoka
Kurasini Dar iliyokuwa inahusu ishu ya mzee moja kudaiwa kuwajeruhi kwa
risasi watu wawili, baadae wakavamia watu ambao walifanya vurugu na
kuchoma moto gari la mzee huyo alafu wakawa wanataka kuchoma moto na
nyumba ya mzee huyo pia.
Mashuhuda walizungumza kuhusu, tuhuma na
lawama zao walizipeleka kwa mzee huyo kwamba ni kawaida yake kuwatishia
bastola watu wanaopita jirani na nyumba yake au wanaompigia kelele.
Leo kasikika mtoto wa mzee huyo ambae
amesimulia hali ilivyokuwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho.. mtoto huyo
amesema kuwa baada ya baba yake kuokolewa na Polisi watu hao walivamia
tena nyumba hiyo wakamjeruhi mtu mmoja ambae aliachwa na Polisi kwa
ajili ya kulinda.. wao walikuwa kwenye uvungu wa kitanda pamoja na ndugu
zake wengine wakati ishu yote inatokea.
Mtoto huyo amesema nao pia walivamiwa na
kundi la watu, wakawa wanatishia kuwanyang’anya simu na pesa, baadae
nao wakaja kuwaokoa, wakatoa na vitu vingine vyote kwenye nyumba.
No comments:
Post a Comment