Tangakumekuchablog
Mkinga, MBUNGE wa jimbo la Mkinga, Dustun
Kitandula, amewataka walimu shule za msingi na sekondari Wilayani hapa
kuzidisha bidii ya ufundishaji darasani lengo likiwa ni kufuta alama ziro.
Akizungumza
katika wiki ya Elimu iliyoadhimishwa Kiwilaya Wilayani humo jana, Kitandula
alisema jitihada zaidi za walimu zinahitajika ili kuziwezesha shule zao kufanya
vizuri katika mitihani ya Taifa.
Alisema
kipindi cha miaka ya nyuma shule za Mkinga zilikuwa zikishika nafasi za mwisho
kimkoa na kitaifa na hivyo sasa walimu
kuonyesha bidii zao darasani ikiwa na panmoja na kuwa na mahusiano mazuri
za wazazi wa wanafunzi.
“Tunatambua kuwa walimu wako na changamoto nyingi shuleni na nje ya
shule----changamoto hii iwe chachu ya kufaulisha wanafunzi na kufuta alama ziro” Alisema Kitandula
Alisema Wilaya ya Mkinga mbali ya kuwa
changa katika sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu lakini inaweza kupiga hatua
mbele katika maendeleo kwa kuwandaa vijana katika elimu ili kuweza kuinua
maendeleo ya Mkinga baadae.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Afisa elimu
Sekondari Wilaya ya Mkinga, Omary Kombo, aliwataka wazazi na walimu kuhakikisha
ujenzi wa maabara unakamilka kama ulivyopangwa.
Alisema kuwepo kwa maabara kila shule
kutasaidia wanafunzi kusoma kwa vitendo pamoja na kufanya vizuri katika masomo
yao ya sayansi na kuondosha uhaba wa walimu wa somo hilo.
Alisema Wilaya ya Mkinga iko na uhaba wa
walimu wa somo la sayansi jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kufanya
vibaya katika mitihani yao ya Taifa.
“Wilaya ya Mkinga iko na uhaba wa walimu wa
masomo ya sayansi----nawaomba wanafunzi muliopo hapa jikiteni katika somo hili
ili kuja kuwasaidieni ndugu zenu hapo baadae” alisema Kombo na kuongeza
“ Nanyi wazazi tushikamane kuwabidiisha
vijana wetu kukosa masomo shuelni kwani huko nje kuna vishawishi vingi kama
uvuaji wa samaki katika bahari yetu tunayopakana nayo” alisema
Aliwataka walimu kuwa na ushirikiano na
wazazi pamoja na kamati zao ili kuweza kuleta maendeleo ya wanafunzi pamoja na
mazingira ya shule na kumaliza majengo ya maabara.
Mwisho
No comments:
Post a Comment