Tangakumekuchablog
Tanga, MSTAHIKI
Meya halmashauri ya jiji la Tanga, Omary Guledi, ameitaka jamii kushikamana na
kuvumiliana kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ili kuliwezesha Taifa
kuvuka kwa amani kipindi cha kampeni na
uchaguzi.
Akizungumza wakati futari
iliyoandaliwa na Bank ya Diamond
Trust Bank (DTB) kwa kushirikiana
na mshirika wake, Express Global Money, Guledi alisema kipindi hiki kuelekea
uchaguzi jamii inatakiwa kuvumiliana na kuitunza amani iliyopo.
Aliitaka jamii kuacha kushabikia
vyama vya siasa hadi kupelekea
kuhasimiana na hivyo kuitaka kupima sera
za wagombea viongozi wenye uwezo
wa kuongoza na wanaoweza kusukuma mbele maendeleo.
“Kupitia hadhara hii ni fursa adhimu
kutoa ujumbe kwa wananchi hasa kipindi hiki tunachoelekea uchaguzi mkuu----kitu
cha msingi zaidi ni suala la amani na utulivu uliopo” alisema Guledi na
kuongeza
“Tuwasikilize wanasiasa
wanavyojinadi na kutoa sera zao ila tuwe makini siku ya kuchagua----tusichague
kwa kuangalia sura wala nasaba kinachotakiwa ni uadilifu na kiu ya maendeleo”
alisema
Aliwataka wananchi kuwapima wagombea
wanaotaka kura zao kwa sera na vipaumbele vyao na kuepuka kuchagua wagombea kwa
kuangalia sura na nasaba jambo ambalo linaweza kuwaongezea umasikini majumbani.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha
masoko Bank ya (DTB) , Sivlester Bahati,
alisema bank hiyo imeviwezesha vikundi mbalimbali vya ujasiriamali wanawake
kuwapa mikopo na kutoa mbinu za kuwa
wajasiriamali wakubwa .
Alisema bank hiyo iko na mikakati ya
kumuenua mwananchi wa kipato cha chini kuwekeza kwa kuweka akiba kadri ya uwezo
wake na kufaidika fursa ya mikopo na bank kumpa mbinu za kuanzisha mradi ambao
atamuwezesha kurejesha rejesho..
“Bank yetu iko na mipango kemukemu
ya kumuenua mwananchi wa kipato cha chini----tunampa elimu ya ujasiriamali na
mbinu ya kuwekeza kasha kukopa na kurejesha” alisema Bahati
Alisema bank hiyo iko na mikakati ya
kufungua matawi kila Wilaya lengo likiwa ni kumfikia mwananchi wa hali ya chini
pamoja na wafanyabiashara ili kuepuka wizi na uporaji .
Mwisho
Waumini wa dini ya Kiislamu na wakazi wa Tanga wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Bank ya Diamond Trust Bank (DTB) kwa kushirikiana na mshirika wao, Express Global Money juzi, ambapo zaidi ya watu 300 walishiriki na kuongozwa na Meya wa jiji la Tanga, Omary Guledi.
No comments:
Post a Comment