HADITHI hii inaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Tiba Asilia Cha Mkombozi Sanitarium Clinic. Mabingwa wa magonjwa sugu na yaliyoshindikana. Mkombozi wa ko na mashine za kisasa za kupima mwili mzima kwa gharama nafuu. Wapo Tanga eneo la Chuda mkabala na Rahaleo. simu 0654 361333
NILIJUA NIMEUA 3
ILIPOISHIA
Aliingia ndani ya teksi
akaichukua ile simu na kutoka.
“Asante kaka. Kumbe ulikuwa
unanitania!”
Sote tukacheka. Huzuni
ilikuwa imeshamtoka.
“Wewe ni muaminifu sana. Nitakuwa nachukua
teksi yako kila siku” akaniambia.
“Kwaheri, nakwenda zangu”
nikamuaga.
“Ulikuwa umeniletea simu
yangu. Asante sana kaka, endelea kuwa na
moyo huo huo”
“Asante bibie”
Wakati natia gea niondoe gari
sauti yake ikanisitisha.
“Nipe namba yako.
Nitakuhitaji tena siku nyingine”
Nikamtajia namba yangu.
SASA ENDELEA
Akaijaza kwenye simu yake.
“Na mimi nipe yako”
nikamwambia.
“Ngoja nikupigie. Unaitwa
nani?”.
“Majombi Teksi”
Jina hilo likamchekesha. Alipolijaza kwenye simu
akanipigia. Simu yangu iliita. Nikaishika na kuitazama.
“Hii ndio namba yako”
“Ndiyo hiyo”
“Unaitwa nani?”
“Mariam” akatamka haraka.
Nikahifadhi ile namba pamoja
na jina lake kwenye simu yangu. Nilipomaliza
nikamwambia “Sawa”
Nikaiondoa teksi.
Huo ukawa mwanzo wa kujuana
na Mariam.
Kutoka siku ile akawa
ananipigia simu mara kwa mara kuniita sehemu kwa ajili ya kuhitaji huduma ya
teksi yangu. Kulikuwa na siku ambayo alinipigia simu saa tisa usiku. Nilikuwa
nimesharudi nyumbani na nilikuwa nimelala. Nikaamka na kuangalia simu iliyokuwa
inaita. Nikaona ni yeye aliyekuwa akinipigia. Nikashituka na kujiuliza kwanini
alikuwa ananipigia simu usiku ule, alikuwa wapi na alikuwa na nini?
“Hallo Mariam …vipi?”
nikamuuliza baada ya kupokea simu yake.
Nilikuwa nimekereka
kukatishwa usingizi wangu lakini nilivumilia.
“Majombi uko wapi?” Sauti ya Mariam ikauliza.
“Niko nyumbani” nikajibu.
“Ninakuhitaji hapa Habours
Club”
Habours ilikuwa klabu ya
starehe ambayo ilikuwa ikitumiwa kwa maonesho ya miziki hasa miziki ya taarab.
“Unataka nikufuate hapo
Habours Club?” nikamuuliza.
“Ndiyo”
“Nikupeleke wapi?”
“Nyumbani”
“Ulikuwa kwenye mziki?”
“Ndiyo”
Nilisita kumpa jibu. Kwa
upende mmoja sikupenda kukatisha usingizi wangu kwani nilihitajika kuamka saa
kumi na mbili asubuhi niingie kazini. Kurudi kwangu nyumbani ni saaa sita au
saba usiku.
Lakini kwa upande mwingine
sikutaka kumkatisha tamaa mteja wangu. Kwa vile ilikuwa ni kazi ya usiku
nilijua ingeniingizia pesa nzuri. Nikaona nimfuate.
“Unasemaje, utanifuata?” Sauti ya Mariam ikakatisha mawazo yangu.
“Mko wangapi?” Nikamuuliza
ili kupanga masilahi yangu.
“Tuko wawili, mimi na rafiki
yangu”
“Nisubirini, nakuja”
“Sasa ukifika nipigie
unishitue kwani tuko ndani”
“Sawa, nitakupigia”
Mariam akakata simu.
Niliondoka kitandani na
kuanza kuvaa. Nilikuwa nikiishi eneo la Msambweni kwenye nyumba yangu mwenyewe.
Ilikuwa nyumba ya urithi. Tuliirithi mimi na mdogo wangu wa kiume baaada ya
baba yetu kufariki dunia.
ITAENDELEA KESHO, usiache ukapitwa na uhobdo huu ni kitafuta, ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment