Breaking News, Okwi ndani ya Denmark kwenye uthibitisho wa picha kabisa..
Siku kadhaa baada ya kumaliza majaribio ya wiki mbili katika klabu ya Sonderjyske inayoshiriki katika ligi kuu ya Denmark, mshambuliaji Emmanuel Okwi amefaulu majaribio hayo.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo ya Denmark, mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa na Simba msimu uliopita akitokea Yanga amejiunga rasmi na timu hiyo baada ya kufuzu majaribio yake.
Okwi
amesaini mkataba wa miaka 5 wa kuitumikia klabu hiyo na leo
ametambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari akikibidhiwa jezi
namba 25.
Mpaka
sasa haijawekwa wazi ni kiasi gani klabu ya Simba imelipwa kuumuza Okwi
ambaye miaka kadhaa nyuma walimuuza kwa Dola 300,000 kwenda klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia kabla hajarejea Tanzani kuitumikia Yanga.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment