SIMULIZI ZA FAKI A FAKI 0655 340572
MWANAMKE 13
ILIPOISHIA
Tukaendelea kusubiri hadi saa
kumi na mbili jioni.
“Sidhani kama atakuja tena”
Kaka akaniambia.
“Basi twenzetu”
“Twenzetu”
Tukanyanyuka.
“Ametupotezea muda wetu bure”
Kaka akasema.
“Nashukuru pia hivyo ambavyo
hakutokea’
Kaka akacheka.
“Kwanini useme hivyo?’
“Yule mwanamke mimi
nilishapanga nisikutane
naye tena!”
“Lakini ndiye aliyekuokoa”
“Kwani yale matatizo si
ameniletea yeye!”
Tulikuwa tumeshatokea
barabarani.
“Naona turudi kwa miguu tu”
nikamwambia kaka.
Tukarudi kwa miguu.
Tulipofika nyumbani kwa mama,
mama akatuuliza.
“Mlikutana naye?”
“Hakuja” nikamjibu.
“Tumekaa mpaka tumechoka”
Kaka akaongeza.
“Kwanini asije na alikwambia
mkutane hapo saa kumi na moja”
“Labda amebadili mawazo”
nikamwambia.
“Ndiyo vizuri”
SASA ENDELEA
“Mimi pia nimemwambia kaka ni
vizuri kama hakuja, simuhitaji. Namuona kama
nduli”
“Ni nduli kweli.
Angekuharibia maisha yako” Mama akaniambia.
“Lakini haikuwa vibaya
kumsikiliza kujua alitaka kukwambia nini” Kaka akaniambia.
“Basi yameshapita”
Baada ya hapo mimi na kaka
tulimuaga mama na kuondoka. Kaka alikwenda kwake na mimi nikarudi nyumbani
kwangu Msambweni.
Nilipofika nilioga.
Nilipomaliza kuoga nilikaa sebuleni na kujiwazia.
Mpaka muda ule nilikuwa siamini kama
niliachiwa na mahakama na nilikuwa huru.
Niliona hivyo kwa sababu
kuachiwa kwangu kulikuwa kwa miujiza sana.
Kila aliyekuwa akisikiliza ile hukumu alijua kuwa nafungwa kwani nisingeweza kupata zile
pesa zilizotakiwa.
Lakini yule mwanamke
alishajua kuwa ningetakiwa kulipa pesa zile na pia alijua kuwa nisingekuwa nazo, hivyo akaja nazo na
kusubiri hukumu.
Kwa upande mwingine nilikuwa
sijajua nia ya yule msichana. Sikujua alikuwa akitaka nini kwangu kwani
hatukuwahi kuwa na makubaliano yoyote tuliyokubalina.
Wakati niko katika lindi la
mawazo sebuleni kwangu simu yangu ya mezani iliyokuwa pembeni mwa sebule
ikaita. Ilinishitua sana.
Simu hiyo ilikuwa haipigwi mara kwa mara. Wakati ule hakukuwa na waswahili
wengi waliokuwa wakimiliki simu hivyo mawasiliano ya simu yalikuwa madogo sana.
Nikanyoosha mkono wamgu na
kukinyakua chombo cha simu cha kusemea.
“Hallow!” nikasema nikiwa
simjui aliyenipigia.
“Hallow!” Sauti nyembamba ya
mwanamke ikajibu kutoka kwenye simu.
“Amour hapa, nani mwenzangu?”
“Unazungumza na Zena”
Moyo wangu ukashituka.
“Nani…Zena?”
“Ndiyo Zena”
Nilishajua kuwa huenda
alikuwa yule msichana wa kijini lakini nilitaka kuthibitisha.
“Zena nani?”
“Ohoo umenisahau leo. Nilikwambia tukutane saa kumi
na moja jioni katika bustani ya Uhuru”
“Ndiyo nilifika na
nilikusubiri lakini wewe hukutokea”
“Ninajua kwamba ulifika na
ulinisubiri lakini mimi sikutokea”
“Kwanini?”
“Umeniudhi”
“Nimekuudhi?”
“Ndiyo”
“Nimekuudhi kwa vipi?”
“Ulikuwa pamoja na nani?”
Nikasita kidogo kabla ya
kumjibu.
“Nilikuwa na kaka yangu”
“Kaka yako mimi namjua?”
“Hapana, hunjui”
“Sasa ulikuja na kaka yako
kwa ajili ya nini?”
“Alikuwa amenisindikiza tu”
“Lakini tulikubaliana
tukutane mimi na wewe. Kwanini ulimleta kaka yako?” Hapa Zena alisema kwa ukali kidogo.
Nikanyamaza.
“Sasa uliyevunja ahadi ni
mimi au wewe?” Zena akaniuliza.
Sikumjibu kitu.
“Sema ni wewe. Mimi nilipoona
umekuja na mwenzako kinyume na makubaliano yetu sikujitokeza”
“Basi nisamehe”
“Nimeshakusamehe ila kuna kitu nataka
kukwambia”
“Fika tena kesho saa nne
asubuhi pale Uhuru
Park”
“Utakuja?”
“Ndiyo nitakuja”
“Sawa, basi nitafika”
“Kwaheri”
Simu ikakatwa.
Niliuweka mkono wa simu
nikawa najiuliza, msichana huyo aliipata wapi namba yangu ya simu. Sikukumbuka
kama niliwahi kumtajia namba yangu ya simu. Kitendo kile cha kunipigia kilikuwa
kimenishitua na kunishangaza.
Sasa nikawa nimetambua sababu
ya Zena kutofika mahali ambapo tuliahidiana kukutana. Kumbe ilikuwa ni kwa
sababu nilikwenda na kaka wakati yeye hakupenda awepo mtu mwingine.
Nikawa nimeshapata wasiwasi, nikavaa nguo na kutoka.
Nilikwenda kwa mama yangu nikamueleza.
Mama akaniambia niende
nikamueleze kaka yangu aliyekuwa akiishi eneo la Chuda,
nikaenda. Ilikuwa karibu saa tatu usiku.
Kaka aliponiona akashituka.
“Vipi ndugu yangu?”
akaniuliza.
“Yule mwanamke amenipigia
simu” nikamwambia.
“Kumbe ulimpa namba yako?”
akaniuliza.
“Hapana, sikumpa”
“Aliipata wapi?”
Nikabetua mabega yangu.
Sijui. Hata mimi mwenyewe nimeshangaa”
“Amekwambia nini?”
“Ameniambia hakutokea kwa
sababu nilikwenda pale nikiwa na wewe”
“Yaani alitaka uwe peke
yako?”
“Ndiyo hivyo”
“Kumbe alituona tuko wawili!”
“Bila shaka”
“Sasa amekwambiaje?”
“Ameniambia tukutane tena
kesho saa nne”
“Kwani anataka nini?”
“Sijajua”
“Sasa wewe umeamuaje?”
“Nataka ushauru wako”
“Mimi nakushauri nenda”
“Basi nitakwenda”
“Kwa sababu hujui anataka
kukwambia nini. Pengine anataka kukwambia kitu cha maana kwako”
“Ni kweli”
“Huwezi jua, anaweza kukupa
utajiri”
“Unasema kweli kaka?”
“Wewe nenda kamsikilize,
usiogope”
“Sawa. Nitakwenda”
Baada ya kuzungumza na kaka
kwa dakika kadhaa nikamuaga.
“Basi kaka mimi narudi
nyumbani”
HII STORI NI KALI SANA! HIVI SASA INATIKISA
NCHI. KILA UNAPOFIKA UNAKUTA WATU WANAIJADILI. WASOMAJI WANAONGEZEKA KWENYE
BLOGY. SI MZHEZO!
BASI TUONANE TENA HAPO KESHO ILI UWEZE KUJUA NINI KITAENDELEA. Fugua blog yako mapema
asubuhi upambane na Zena.
No comments:
Post a Comment