Tuesday, June 7, 2016

WANYAMA WAKALI LIVE MAONYESHO YA MWAHAKO TANGA

 Ni watu wachache wenye uelewa maana ya Maonyesho ya Biashara pale yanapofanyika eneo husika. Maonyesho ni fursa kwa kila mtu kujionea mambo mbalimbali uyajuayo na yale ambayo hujawahi kuyaona mbali ya kuona katika Luninga za ndani na nje ya nchi.
Ni maonyesho ya siku 10 ambayo yamefikia tamati jana Mwahako nje kidogo ya jiji la Tanga ambapo wakazi wa Tanga wamejionea Live wanyama wakali ambao ni hatari akiwemo Simba, Chui, Twiga, Faru, Kiboko, Swala na wengine wengi ambao wanajulikana kwa ukali porini.
Ajabu ya wanyama hao kujiuliza kuwa walifikishwaje katika maonyesho hayo ilhali Simba anatmbulika kwa ukali na inadaiwa hula watu pamoja na Chui.
Wanyama hao waliingizwaje katika mabanda na walikuwa watu wangapi ambao hawakuogopa kuliwa na Simba au Chui.
Cha ajabu wahuduma wa Maliasili na Utalii ambao walikuwa wakielimisha wananchi waliofika katika maonyesho hayo walikuwa wakiwaita Simba kwa majina ambayo wamepewa na akitakiwa kulala hulala na kusimama husimama.
Baadhi ya watu waliozungumza na tangakumekuchablog wamesema wamefurahishwa sana kwani katika maonyesho mengi hawakuweza kuona wanyama hao zaidi ya bidhaa za majumbani na urembo mwengine wa kumpendezesha mtu.
 Chui akihaha kutaka kutoka katika banda
 Simba mkali akiwa ametega na kujifanya amelala na kumsubiri mtu tu anyooshe mkono aukwapue na kuula.

 Hapo hajalala ila anakula taimingi ya mtu achomoze mkono na kuula kwani yuko na kasi zaidi ya spiti mia tano.



 Anatisha na ni mpole kumbe ni mkali hatari
 Baadhi ya wakazi wa Tanga wakichukua picha kw atahadhari kubwa kwani Simba huyo mbali ya kujengewa kwa vyuma lakini yuko na nguvu za kuking'oa na kuingia mitaani na kuwa hatari

Huyo ni Koongo joka.

No comments:

Post a Comment