Kifo cha Mohammed Ali chazua siasa Marekani
Kifo cha Muhammed
Ali kimezua malumbano makali katika ulingo wa kisiasa miongoni mwa
wagombea wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu, utakaofanyika mwezi
Novemba nchini Marekani.
Katika risala zake za rambirambi mgombea
wa kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump,
amesema kuwa Ali kwa hakika alikuwa Bingwa ambaye atakumbukwa na wengi.Mwaka Jana, Ali alilaani wito uliotolewa na Trump, ya kuwazuia kabisa waislamu kuingia nchini Marekani.
Kwa upande wake mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, Seneta Bernie Sanders, amemshutumu Trump na kumtaja kuwa mnafiki.
Naye Hillary Clinton, amesema kuwa Trump, anafaa kuhukumiwa kwa matamshi yake anayotoa.
Bondia huyo alifariki siku ya Ijumaa huko Arizona, na alikuwa akiugua maradhi ya kusahau- sahau, kwa zaidi ya miaka thelathini.
No comments:
Post a Comment