Ng'ombe aliyesakama kichwa chake ndani ya mti mkubwa ameokolewa.
Haijulikani ni vipi ng'ombe huyo aliingiza kichwa chake ndani ya mti huo. Waokoaji wakishirikiana na wazima moto na daktari wa
wanyama walishughulika kumuokoa ng'ombe huyo ambaye kichwa chake
kilikuwa ndani ya mti katika kitongoji cha North Yorkshire. Mmiliki wa ng'ombe huyo aliomba msaada wa dharura
Northallerton na shughuli hiyo iliposhindwa kumnusuru ng'ombe wake
ikawabidi kuwahusisha wazima moto waliotumia msumemo maalum wa mduara
kukata kwa ueledi mti huo bila ya kumjeruhi na kisha
wakamnusuru.
Alikuwa akitupa mateke ilimbidi afisa anayewatibu mifugo kumdunga sindano atulie ili shughuli hiyo ifanikiwe. .
Baada ya muda ng'ombe huyo aliokolewa.
No comments:
Post a Comment