Monday, June 6, 2016
TAMBI , FUTARI
Mfanyabiashara soko la Ngamiani Tanga, Adam Bakary, akipima tambi kwa wateja, Mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani kwa Waislam tambi hutumika kama moja ya futari.
Waislamu kote Duniani wameianza funga ya Ramadhwani ikiwa ni kutekeleza moja ya nguzo kuu ya Imaani ambapo hujizuia kula , kunywa na kufanya jambo lolote baya lililokatazwa ndani ya Uislamu.
Ndani ya mwezi huo kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakipandisha bei vyakula masokoni na madukani jambo ambalo limekuwa likiwapa wakati mgumu wafungaji ikiwa ni kujipatia pesa kwa njia za hila.
Hali hiyo ambayo baadhi ya Wafungaji wameiambia tangakumekuchablog kuwa ni vyema tume ya kudhibiti bei kutembelea masokoni na madukani na kukomesha hali hiyo ambayo imekuwa sugu kila vipindi vya mfungo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment