Mkataba mpya wa Azam TV na TFF umetangazwa leo July 12
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF
leo July 12 2016 limetangaza good news kwa mashabiki wa soka ambao
huenda huwa wanakosa muda wa kwenda uwanjani kuangalia mechi, TFF leo imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitano na Azam TV kwa ajili ya kuendelea kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara.
Mkataba huu wa Azam TV
sasa klabu itakuwa inapewa milioni 126 kwa awamu tatu tofauti na awali
ilivyokuwa milioni 100, awamu ya kwanza na pili zitatolewa milioni 42,
halafu awamu ya mwisho klabu inayomaliza nafasi za juu zaidi inalipwa
zaidi kuliko iliyopo nafasi ya chini, hii inatokana na TFF na Azam TV kuamua kuleta ushindani.
No comments:
Post a Comment