Saturday, July 2, 2016

MAREKANI YATOA TAKWIMU ZA WATU WALIOKUFA KTK NDEGE ZISIZO NA RUBANI

US yatoa idadi ya watu waliouawa na ndege zisizo na rubani

Ndege zisizo na rubani

Serikali ya Marekani imetoa makadirio rasmi ya idadi ya raia ambao huenda waliaga dunia katika mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani za Kimarekani, tangu rais Barrack Obama aingie mamlakani.

Idadi hiyo ni takriban watu 64 hadi 116, japo haijahusisha mataifa kama vile Syria, Iraq na Afghanistan.

Mataifa yaliyojumuishwa ni Pakistan , Yemen na Somalia ambapo Marekani imekuwa ikilenga makundi ya kigaidi na watu binafsi.

Makundi ya wanaharakati wa haki za kibinadam yanasema idadi halisi ni kubwa kuliko iliyotolewa na Marekani.

No comments:

Post a Comment