Mwanamfalme Philip amuoa muigizaji Sweden
Mamia
ya watu wamejitokeza mabarabarani mjini Stockholm Sweden kushuhudia
harusi ya mwanamfalme Prince Carl Philip na muigizaji nyota na
mwanamitindo wa zamani Sofia Hellqvist.
Harusi yao ilifanyika leo adhuhuri katika makao ya kifalme mjini Stockholm.Sofia Hellqvist, 30, alikuwa mkufunzi wa yoga na mwanamitindo kabla ya kuanzisha shirika lisilokuwa la kiserikali.
Mumewe 36 Carl Philip, Mwanamfalme ni watatu katika orodha ya familia ya kifalme mwenye uwezo wa kutawala Sweden.
Wawili hao wanasemekana kuwa walionana mara ya kwanza katika mkahawa mmoja mwaka wa 2010.
Takriban wageni mashuhuri 200 walihudhuria chajio na maharusi hao katika kisiwa cha kifahari cha Skeppsholmen.
No comments:
Post a Comment