HADITHI na Faki A Faki , 0713 340572 , 0655 340572
MWANAMKE ALIYENICHUNUKA 11 inaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Tiba Cha Mkombozi Sanitarium Clinic Tanga, Mkombozi wako na vifaa vya kisasa vya kupimia mwili mzima na kutoa ushauri wa kitaalamu, simu 0654 361333
ILIPOISHIA
”Kama
wewe ni Mtemi Wembe, mimi ni Banuna mwana wa Ziraili…mimi wa ukoo wa kifalme.
Wewe huwezi kuniita mimi….”
“Nakwambia…..!” Mtemi wembe
alitaka kusema lakini Banuna hakumpa nafasi.
“Una shida gani na mimi?”
akaendelea kumuuliza kwa sauti yake kali na ya kiburi.
“Nataka kukutenganisha na
Alfred, leo iwe mwisho wako kumfuata!” Mganga akamwambia kwa sauti kali.
Bananuna kwa jeuri alikishika
kiuno chake akamwambia mganga.
“Nakwambia huniwezi! Alfred
nitakuwa naye hadi kifo chake. Simuachi! Unasemaje?”
Hapo hapo mganga naye
akapandisha jini lake.
“Shiit! Wewe nani Tanzania?
Utakwenda tu!. Leo nitakuondoa kwa sababu umekosa adabu!” Jini wa mganga huyo
akasema kwa ghadhabu.
SASA ENDELEA
Nikajiambia kimoyomoyo, leo
patazuka balaa! Kabla sijamaliza kuwaza, Banuna alishavuta mkono, akamtandika
Mtemi Wembe kibao cha shavu. Mtemi Wembe akaanguka chini. Hakuinuka tena. Povu
likawa linamtoka mdomoni.
Kitendo hicho kilitufanya mimi,
Juma na wasaidizi wa mganga huyo tukurupuke na kutimua mbio. Juma na mimi
tulitimua mbio za ajabu. Kila mmoja alikimbilia upande wake. Tulikuja kukutana
barabarani.
Kwa sekunde kadhaa tulikuwa
tumesimama tukihema, hatukuweza kuzungumza lolote. Punde tu ikatokea daladala
ikielekea mjini, nikaipungia mkono. Daladala hiyo iliposimama tukajipakia.
Humo ndani ya daladala pia
hatukuzungumza kitu. Kila mtu aliyetuona alijua kuwa tumepatwa na jambo tena
jambo kubwa.
Tulipofika stendi ya Tanga
tulishuka. Mwili wangu ulikuwa bado ukutetemeka. Juma akanitazama kisha
akatikisa kichwa kusikitika.
“Ni hatari!” akaniambia na
kuongeza.
“Sikutarajia kuwa yatatokea
mambo kama yale!”
“Mimi nilikuwa na mashaka
tangu mapema”
“Yule msichana aliyekuja pale
na kumpiga yule mzee ni nani?”
“Si ndiye huyo jini
anayenifuata!”
“Kumbe jini mwenyewe ndiye
yule, mkali namna ile!”
“Umemuona mwenyewe Juma!”
“Kwa uzuri ni mzuri sana lakini anatisha.
Sijui kama yule mganga atapona!”
“Kama
mganga mwenyewe amepigwa, je mimi mwenyewe itakuwaje!”
“Na ni mganga niliyemtegemea sana. Inaonesha tatizo
lako ni kubwa sana”
“Sasa tufanyeje rafiki
yangu?”
“Twende nyumbani,
tutashauriana”
Tulipofika nyumbani kwa Juma,
tulikaa na kuanza kujadiliana.
Juma aliniambia kuwa yule
mganga ameshashindwa na haitakuwa na maana yoyote kurudi kwake tena. Na kama ni suala la pesa zetu tulizompa ndio zimeshapotea.
Tusingeweza kwenda kumdai. Na pia hatukujua hali yake itakuwaje.
“Kwa jinsi hili tatizo
lilivyo, mimi ningekushauri uende Pemba. Kule
kuna waganga hodari sana
wa majini”
“Hata mimi nimewahi kusikia
hivyo”
“Nimesikia wanawafuga majini
majumbani na kuwatuma”
Sikumjibu kitu. Nilikuwa
nikiwaza jinsi nitakavyofika huko Pemba wakati
sikuwa na akiba yoyote ya pesa.
“Mimi nadhai Alfred uende Pemba” Juma akaendelea kuniambia.
“Ushauri wako ninaukubali,
lakini sina pesa, nitakwendaje?”
“Hilo nalo ni tatizo jingine. Itabidi tusubiri
mwisho wa mwezi nikupe mshahara wangu”
“Halafu wewe utatumia nini?”
“Usijali Alfred, nitakopa
kopa hivyo hivyo”
Kwa kweli nilihuzunika sana lakini sikuwa na
jinsi.
“Usihuzunike rafiki yangu.
Yote yatakwisha. Hakuna lisilo na mwisho”. Juma akaniambia kwa moyo wa huruma.
Kutokana na hofu niliyokuwa
nayo kuhusiana na Banuna, niliendelea kuishi kwa Juma nikisubiri mwisho wa
mwezi ufike anipe mshahara wake niende Pemba kutafuta
waganga. Lakini kutoka siku ile tuliyokwenda Amboni kwa yule mganga na kutokea
lile tukio, sikumuona tena Banuna.
Usiku mmoja wa kuamkia ile
siku ambayo Juma angepata mshahara wake na kunipa kama
alivyoniahidi, lilitokea tokeo ambalo sitalisahau.
Usiku
huo nilikuwa nimelala na Juma, nilishituka usingizini na kumuona Banuna
amesimama kando ya kitanda upande ninaolala mimi. Alikuwa amevaa nguo nyeupe
tupu. Ilikuwa ni hali ambayo ingenifanya nishituke na pengine kupiga kelele au
kutoka mbio.
Lakini
sikushituka wala sikupiga kelele wala sikutoka mbio. Nilikuwa kama zezeta.
Nilijiona kama nilikuwa katika ndoto kwani akili hazikuwa zangu.
“Alfred!”
Banuna akaniita alipoona nimeamka.
“Ndiyo
Banuna!” nikamuitikia kwa sauti tulivu.
“Umeniona?”
akaniuliza kama aliyekuwa ananisomesha.
“Ndiyo
nimekuona, si Banuna wewe?”
“Nimekufuata
twende kwetu”
“Kwenu
wapi?”
“Kwetu
baharini. Uko tayari twende?”
“Niko
tayari” nikamjibu”
“Amka
basi twende zetu”
Nikainuka
na kushuka kitandani. Juma alikuwa amelala fofofo.
“Vaa
nguo zako” akaniambia.
Nikavaa
suruali, shati na viatu.
“Sasa
twende”
Akanishika
mkono.
Tukatoka
mle chumbani. Akafungua mlango wa mbele na kuniambia nitangulie kutoka nje.
Nilipotoka na yeye akafuatia.
Aliinama
chini akachora msitari mbele yangu kisha akaniambia.
“Vuka
huo msitari”
Nikiwa
kama zezeta ambaye sikuwa na uwezo wa kuwaza chochote, nilitii alichoniambia,
nikapiga hatua na kuvuka ule msitari. Kufumba na kufumbua nikajiona niko katika
eneo jingine ufukweni mwa bahari. Banuna alikuwa amesimama kando yangu,
akanishika mkono na kuniambia.
ITAENDELEA
KESHO hapahapa Tangakumekuchablog
| |||||||||||||||||
Tuesday, April 12, 2016
HADITH MWANAMKE ALIENICHUNUKU SEHEMU YA ( 11 )
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment