Makonda Apiga Marufuku Wananchi Kuwapa Pesa Omba Omba Barabarani
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepiga marufuku wanaotoa Pesa kwa Omba omba kando ya barabara kwa kuwa wanachangia uwapo wa watu hao huku baadhi ya watu wakiwatumia watoto hao kujipatia kipato kinyume cha sheria.
Akizungumza jijini Dar es salaam Makonda amesema kumekuwa na Ongezeko kubwa la watoto katika barabara kadhaa za jiji la Dar wakijihusisha na Kuomba pesa huku wanaowatuma wakiwa wamekaa pembeni jambo ambalo ni kinyume na sheria lakini pia linahatarisha Usalama wa watoto hao.
Vilevile amesema mkakati uliokuwapo kwa kushirikiana na Ustawi wa jamii, Tamisemi pamoja na manispaa kuhakikisha kuwa watoto hao wanakusanywa na kuwekwa katika vituo maalum huku wanaohusika na kuwatumia kufanya kazi hiyo wakichukuliwa hatua.
No comments:
Post a Comment