Tangakumekuchablog
Tanga, NAIBU
Waziri wa Afya, Hamis Kigwangala, amewataka Madaktari na Wakuu wa Idara katika
hospitali nchini kufanya kazi kwa bidii na kusema kuwa Serikali inataka kutumia
mfumo wa Elekronic na kuondokana
na makaratasi.
Akizungmza na madaktari na
wafanyakazi wa hospitali ya Bomb oleo wakati wa ziara yake ya kujionea utendaji
kazi na changamoto zinazowakabili, Kigwangala amesema Serikali ya awahi ya tano
haitaki wafanyakazi wazembe.
Amesema kila mtumishi anapaswa
kufanya kazi kwa weledi ili kuondosha manung’uniko ya wananchi hivyo kuwataka
kujituma.
Amesema Serikali inataka kuondosha
mfumo wa kuweka kumbukumbu katika makaratasi na badala yake kuweka kwa mfumo wa
Elektoroniki ili kuweza kufanya kazi kwa
wepesi na weledi.
Naibu huyo amefurahishwa na
mazingira ya hospitali hiyo na kusema kuwa jitihada zinatakiwa kuongezwa ikiwa
na pamoja na kuwahudumia wagonjwa.
Mwisho
Naibu
Waziri wa Afya, Hamis Kigwangala, akishuka ngazi kutoka wodi ya watoto
hospitali ya Bombo wakati alipofanya ziara yake leo.
Katibu wa Afya hospitali ya Bombo Tanga, Adam Katundu, akitaka ufafanuzi wa jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Hamis Kigwangala wakati alipofanya ziara hospitalini hapo leo.
Daktari hospitali ya Safi Medics ya Tanga, Joseph Mbaresero, akiuliza swali kwa Naibu Waziri wa Afya, Hamis Kigwangala, wakati alipofanya ziara hospitali ya Bombo leo.
No comments:
Post a Comment