Tuesday, April 12, 2016

MTU MREFU ZAIDI DUNIANI ALIZIZIMISHA JIJI LA MAURITIUS

Mtu mrefu zaidi duniani raia wa Uturuki Sultan Kösen aliye na urefu wa futi 8 na inchi 3 au mita 2.51 amewasilia nchini Mauritius leo asubuhi.

Sultan alilakiwa na umati katika kisiwa hicho cha bahari ya Hindi, kwa mujibu wa taarifa zilizowekwa kwenye ukusara wa facebook wa mtandao wa habari wa nchi hiyo.




Sultan mara ya kwanza alitajwa kuwa mtu mrefu zaidi duniani mwaka 2009 wakati alitimia urefu wa futi 8 na inchi moja mwaka 2009.

Akiongea wakati aliingia kwenye rekodi ya kitabu cha Guinness World Records alismea," Singetarajia ningekuwa kwenye kitabu hicho, nikuwa na ndoto lakini bado ulikuwa ni mshangao mkubwa.
Sultani alilakiwa na maelfu ya Raia waliofika kumuona na kusema kuwa amefarijika sana kwa mapokezi hayo alodai kuwa si chenginecho bali ni watu kutaka kumuona yeye hasa ikizingatiwa amekuwa gumzo duniani kote.

No comments:

Post a Comment