ETHOPIA YANUNUA NDEGE YA KISASA, YATUA KENYA KWA MARA YA KWANZA
Ndege ya kisasa ya Ethiopia yatua Kenya
Ethiopia imekuwa taifa la kwanza barani Afrika kununua ndege ya kisasa aina ya Airbus A350 XWB.
Ndege hiyo, Airbus A350, ndiyo ya hivi karibuni kuzinduliwa na kampuni ya ndege ya Airbus ya Ufaransa.
Ndege
hiyo, iliyo na uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 300, ilitua katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya
Jumatano jioni ikitokea mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Ndege hiyo ni ya kwanza kuwasilishwa kwa kampuni hiyo,
huku nyingine 13 ilizoagiza kutoka kwa kampuni ya Airbus zikisubiriwa
hivi karibuni.
Safari ya kwanza ya ndege hiyo ilifanyika tarehe 2 Julai iliposafiri kutoka Ufaransa hadi mjini Lagos, Nigeria. Viwango vya juu vya teknolojia iliyotumika kuunda
ndege hiyo, vinachangia katika kuinua utendakazi wake, kupunguza
matumizi ya mafuta pamoja na kupunguza kwa kiasi kikubwa utoaji wa hewa
chafu
Kampuni ya Ethiopian Airlines inaorodheshwa ya kwanza barani Afrika kwa faida na pia idadi ya maeneo inayosafirisha abiria. Mwaka wa 2012, shirika hilo pia lilikuwa la pili
duniani na la kwanza barani afrika kununua ndege aina ya Boeing 787
Dreamliner, ya kampuni ya Boeing, yenye afisi zake kuu Chicago,
Marekani. Kampuni ya Airbus na Boeing zinaongoza duniani
katika utengenezaji wa ndege za kisasa, japo Airbus ina umaarufu mkubwa
na imeipiku Boeing kwa faida na uuzaji wa idadi kubwa ya ndege.
No comments:
Post a Comment