Monday, July 11, 2016

KOREA KASKAZINI YAKATISHA MAWASILIANO NA MAREKANI

Korea Kaskazini yakata mawasiliano na Marekani

Maafisa wa runinga inayothibitiwa na serikali ya Korea Kaskazini, wanasema kuwa serikali ya nchi hiyo itakata mawasiliano na Marekani.
Korea Kaskazini inasema kuwa utawala wa Washington tayari umefahamishwa sababu ya hatua hiyo.
Aidha Korea imesema kuwa maswala ambayo bado yanajadiliwa ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa wamarekani wawili sasa yatajadiliwa chini ya sheria kali za kivita.
Korea Kaskazini inasema hatua hiyo imeafikiwa katika kile kinachotajwa kama sheria ya kivita.
Shirika hilo la sereikali aidha linasema kuwa imeafikia hatua hiyo baada ya Marekani kumuorodhesha rais wa nchi hiyo Kim Jong-un katika orodha ya wale waliopigwa marufuku kutokana na rekodi mbaya ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu.
Wakati huohuo Korea Kaskazini imeapa kudungua manuari yeyote ya kivita itakayolenga roketi zake za masafa marefu.
Marekani na Korea Kusini zimetangaza mipango ya kuweka Mfumo wa ulinzi wa Terminal High Altitude Area Defense (THAAD) unaolenga kudungua makombora ya masafa marefu ya Korea kaskazini..
Korea kaskazini imeonya kuwa hilo ni dhihirisho la mataifa hayo kuichokoza na hivyo kutangaza vita dhidi yao .
Hata hivyo haijajulikana Marekani na Korea Kaskazini zitaiweka wapi mtambo huo wa ulinzi wa kisasa na yupi kati ya washirika hao wawili watauendesha mtambo huo wenye uwezo mkubwa wa ulinzi dhidi ya Makombora.
BBC

No comments:

Post a Comment