Maamuzi ya mwisho ya mahakama kuhusu kesi ya Oscar Pistorius
Mwanariadha mlemavu wa miguu wa Afrika
Kusini Oscar Pistorius leo amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela kwa kosa
la mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp. Mwanariadha huyo tayari
ameshatumikia kifungo cha takribani miezi tisa jela katika kosa la awali
wakati alipopatikana na hatia ya kuua bila kukusudia mwaka 2013.
Kwa sasa kifungo chake kimeongezeka
baada ya upande wa serikali kushinda rufaa hiyo ambapo kosa lake
lilibadilika na kuwa kosa la kuua kwa kukusudia.
Hata hivyo katika tukio la aina yake
mwezi uliopita wakati wa kusikilizwa kwa shauri hilo kuhusu adhabu
aliyopewa mwanariadha huyo alishauriwa na timu ya wanasheria wanaomtetea
walimshauri kuvua miguu ya bandia na kutembea kwenye chumba cha
mahakama bila miguu hiyo.
Hatua hiyo ya kuvua miguu ya bandia
iliyomfanya ashindwe kusimama vizuri ilikuwa na lengo la kumshawishi
jaji ili auone udhaifu wake na kuamua ama amhukumu kutumikia jela kwa
muda wote huo au la.
Hata hivyo upande wa mashtaka ulitoa
hoja na kusema ulemavu wa mwanariadha huyo si jambo la msingi. Ambapo
waliikumbusha mahakama kwamba Oscar Pistorius alimfyatulia risasi mpenzi
wake Reeva Steenkamp mara nne alipokuwa amejifungia maliwatoni.
No comments:
Post a Comment