Thursday, July 14, 2016

TANZANIA KENYA ZAPANDA VIWANGO VYA FIFA

Orodha ya FIFA: Kenya na Tanzania zapanda

Kenya imepanda hatua 43 katika orodha ya hivi punde zaidi ya shirikisho la soka duniani FIFA na kuorodheshwa katika nafasi ya 86 duniani.
Hii ni kwa mujibu wa orodha ya FIFA inayoonesha kuwa Algeria imesalia kidedea barani Afrika japo inaorodheshwa katika nafasi ya 32 duniani.
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ndiyo inayoongoza katika kanda ya afrika mashariki na kati.
DR Congo imeorodheshwa katika nafasi ya 59 duniani na 9 barani Afrika.
Uganda Cranes inaorodheshwa katika nafasi ya 15 barani Afrika na nafasi ya 69 duniani nafasi mbili mbele ya vigogo ya soka barani humu Nigeria.
Kenya ambayo ndilo taifa lililoimarika zaidi inaorodheshwa katika nafasi ya 86.
Harambee stars ya Kenya iliyojifurukuta na kuilaza Congo Brazzaville iliimarika hatua 43 na kuingia chini ya mataifa bora 100 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi sita.
Aidha hii ndiyo nafasi ya juu zaidi kwa Kenya tangu mwaka wa 2008.
Amavubi Stars ya Rwanda imeshuka hatua 8 na kuorodheshwa katika nafasi 111 duniani.
Licha ya kupanda hatua 13, Taifa Stars ya Tanzania inaorodheshwa katika nafasi ya 123
Inafatwa kwa karibu na Burundi ambayo vilevile imepanda hatua 7 na kutimia nafasi ya 125.
Ethiopia ni ya 132,
Sudan 142
Sudan Kusini 153
Mataifa ya mwisho kabisa katika orodha hiyo ya FIFA ni mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki yaani Djibouti, Eritrea na Somalia ambazo zote zinaorodheshwa katika nafasi ya 205.
Argentina ingali inaongoza duniani ikifwatwa na Ubeljiji.
Orodha ya mataifa kumi bora barani AfrikaAlgeria (32)
Ivory Coast (35)
Ghana (36)
Senegal (41)
Misri (43)
Tunisia (45)
Cameroon (53)
Morocco (54)
DR Congo(59)
Mali (61)
Orodha ya mataifa kumi bora duniani1 Argentina
2 Ubeljiji
3 Colombia
4 Ujerumani
5 Chile
6 Ureno
7 Ufaransa
8 Spain
9 Brazil
10 Italia

No comments:

Post a Comment