Wakazi wa Tanga wakiangalia Mbuzi katika moja ya mabanda ya mbuzi Mwanzange ambao watawafaa kwa ajili ya kuchinja kusherehekea Sikukuu ya Idd El Firti ambayo itaadhimishwa wiki hii Duniani kote ikiwa ni kumalizika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Vipindi vya Sikukuu jamii kubwa hupendelea kuchinja mbuzi na kutajwa kuwa ni moja ya vitoeleo bora na vizuri.
Tangakumekuchablog ilifanya ziara katika mabanda mbalimbali ya kuuzia mbuzi na kugundua hadi kufikia leo Mbuzi mmoja alikuwa akiuzwa 60,000 hadi 90,000 kulingana na ukubwa wake.
Safi sana atatufaa na watoto wangu huyu mbuzi, ni ishara ya mteja baada ya kununua mbuzi banda la Mwanzange Tanga leo.
No comments:
Post a Comment