Mafuriko makubwa yaliyoikumba mji mkuu wa Georgia, Tbilisi punde ,yamesababisha maafa makubwa huku watu 8 wakithibitishwa kufariki.
Yamkini wenyeji wa mji huo
wameombwa kukaaa majumbani mwao baada ya wanyama waliohifadhiwa katika
hifadhi moja katikati ya mji huo kusombwa na mafuriko.
Wanyama waliotoweka ni pamoja na simba marara simba wa mwituni,dubu na hata mbweha.
Kati ya wale waliouawa watatu walipatikana ndani ya hifadhi hiyo ya wanyama. .Makundi
ya waokoaji yameanza kutembea nyumba hadi nyengine wakitafuta kuwaokoa
manusura na kutathmini hasara iliyotokea baada ya mvua kubwa kunyesha..Meya wa mji huo Davit Narmania amesema hali ni mbaya mno huku akiwaasa
wenyeji wakae majumbani mwao ilikuzuia matukio ya uvamivizi wa wanyama
pori.
Afisa katika Ofisi ya meya wa mji huo anakadiria hasara iliyotokea kuwa ni ya kima cha dola milioni kumi
No comments:
Post a Comment