Maafisa
wa utawala nchini Pakistan wametoa onyo kwa wazazi watakaokataa kuwapa
watoto wao chanjo ya Polio kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Maafisa
wa utawala katika jimbo la Baluchistan, wanasema
kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuenea upya kwa ugonjwa huo
hatari na hivyo kuwalazimu kuchukua tahadhari zaidi.
Wazazi wengi wanashuku kuwa chanjo hiyo ni
sehemu ya njama ya mataifa ya Magharibi kupunguza idadi ya Waislamu
Kulingana na mpango huo mpya,
kila mtoto atalazimika kuwa na cheti cha kuonesha kuwa tayari amepokea
chanjo hiyo ya kupooza kabla ya kupokea huduma yeyote kutoka kwa Serikali ikiwa ni pamoja na kuingia shuleni. Familia nyingi zinapinga watoto
wao kupokea chanjo kufuatia uvumi kuwa ni njama ya mataifa ya magharibi
ya kuwahasi watoto wao kwa nia ya kupunguza idadi ya waislamu duniani. Kwa habari matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment