Kikosi cha African Sports cha Tanga kilichoinyoa timu ya Kagera Sugar kwa kuitungua bao moja bila Uwanja wa Mkwakwani. Timu hiyo imejiweka katika safari ya matumaini endapo itaibuka na ushindi katika mechi zake zilizobaki na kuepuka janga la kushuka daraja.
Wachezaji wa Kagera Sugar wakiomba dua kabla ya mchezo wao na Timu ya African Sports ya Tanga uwanja wa Mkwakwani na kutunguliwa kwa bao moja bila. Mbali ya kucheza kandanda safi kipindi cha pili lakini timu hiyo bahati haikuwa yao ambapo michomo mingi ilipanguliwa na kipa wa African Sports.
Kipindi cha kwanza timu hiyo ilicheza fyongo na wapinzani wao kuzitumia vyema nafasi hizo na kufanikiwa kupara bao moja dakika ya 34 lililofungwa na Ntala.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment