Ibada ya ukumbusho
iliojawa na mihemko ya aina yake kwa bondia Mohammed Ali imefanyika
katika mji alikozaliwa wa Louisville, Kentucky.
Umati watu 14000 ulisikiliza kwa makini watu wa
tabaka na dini tofauti wakimuomboleza mohammed ali kutokana na umahiri
wake katika ulingo wa michezo na pia alivyoitunza jamii, huku wakisifu
mchango wake katika kuimarisha amani duniani na haki za binadam. Mkewe Ali, Lonnie Ali, anasema mumewe alikabiliwa na
masaibu si haba, bila kuonyesha hasira, na kuwataka watu kufuata mfano
wake. Katika taarifa, rais wa Marekani Barrack Obama,
alimtaja Ali kama mtu shupavu, aliyeng'aa na aliyekuwa na ushawishi
mkubwa kuliko mtu yeyote wa kizazi chake.
Rais wa zamani Bill Clinton, alikumbuka utanashati,
ucheshi na utu aliooonyesha marehemu Ali, wakati akikabiliana na
machungu ya ugonjwa uliomdhoofisha.
BBC
No comments:
Post a Comment