Tangakumekuchablog
Korogwe, DIWANI
wa kata ya Kerenge halmashauri ya Korogwe mjini, Shebila Said Shebila (CCM),
amewataka wanachama wa Vikoba Upendo Tupendane cha Mazinde Tarafa ya Mombo
kushikamana na umoja wao na kuyafikia malengo waliyojiwekea.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa
wanachama wa vikoba Mazinde jana, Shebila alisema umoja huo ni mfano kwa wanawake
wengine kujiunga kwani mbali ya maendeleo waliyopata pia wamekuwa chachu ya
maendeleo Mombo.
Ameitaka Serikali kutuma wataalamu
wa elimu ya vikoba ili wakulima na wajasiriamali wa kazi za mikono kujiunga na
kuweza kufaidika na mikopo ya kukopa na kulipa.
“Kabla ya kuja hapa nilikuwa
nazisikia sifa zenu na najua nini mumefanya na leo mumesimama hapa, kwa
jitihada zenu na umoja wenu nina imani kila mmoja hapa baada ya mwaka mmoja
atakuwa ni tajiri wa mfano” alisema Shebila na kuongeza
“Muko wanachama zaidi ya mia na
ukiangalia kuna wengine wanajiunga huu ni mtaji tunaoweza kusema jiunge
utajirike hongereni sana” alisema
Diwani huyo amevishauri vikundi
hivyo kuwa wabuni miradi mengine zaidi na halmashauri itawasaidia kwa hali na
mali kuhakikisha unakomesha umasikini majumbani.
Alisema Tarafa ya Mombo vijijini vya
Mazinde viko na rasilimali nyingi za kujikwamua na umasikini kikiwemo kilimo
cha matikiti maji na zao la mkonge hivyo kujiunga na vikundi ni njia rahisi
kujipatia fursa za mikopo.
Kwa upende wake wa Kikoba Tupendane,
Issa Sigge, amemtaka diwani huyo kupata
asilimia 20 ya halmashauri kwa vijana na vikundi ili kuimarisha vikundi vyao na
kupunguza wimbi la watu wasio na kazi.
Alisema kuna vijana wengi wamekaa
bila kazi ya kufanya hivyo kuipata asilimia hiyokuanweza kuwavutia vijana na
kuondosha wimbi la wasio na kazi Mazinde jambo ambalo litawasukuma katika kazi
za ujasiriamali.
“Mhshimiwa diwani hebu katupigie
chapuo kule katika mabaraza yenu ya madiwani kuipata ile asilimia 20 ya
halmashauri, hii itawasukuma vijana na wasio na kazi kujiunga na vikundi”
alisema Segga
Segga aliwataka wanachma wa vikoba
kudumisha umoja na mshikamano ili kuweza kuyafikia malengo yao na kuhakikisha
kila mwanachama anawasilisha michango yake kwa wakati.
Mwisho
Wanachama wa Vikoba Tupendane Mazinde Wilayani Korogwe Mkoani Tanga wakionyesha pesa walizochanga wakati wa mkutano mkuu wa Umoja huo uliofanyika Mazinde jana. Jumla ya shilingi milioni moja laki mbili zilichangwa.
No comments:
Post a Comment