HADITHI na Faki . A. Faki simu 0713 340572 au 0655 340572
MWANAMKE
ALIYENICHUNUKA
9
IILIPOISHIA
JANA
Siku
ile sikutoka tena mle chumbani mpaka Juma aliporudi jioni. Alikuta nilikuwa
nikitetemeka kwa homa.
“Alfred
unaumwa?” akaniuliza.
“Nasikia
homa”
“Tangu
saa ngapi?”
“Tangu
asubuhi”
“Dah!
Umeshakula dawa?”
“Bado.
Kwanza hebu kaa nikueleze yaliyotokea kule kwa
mganga”
Huku
akionekana kupata wasiwasi, Juma alikaa kwenye kiti. Nikamueleza yale
yaliyonitokea kule Amboni na nilivyorudishwa nyumbani kimiujiza.
Juma
akashangaa.
SASA
ENDELEA
“Sasa
baada ya tukio hilo
umefanya nini?” akaniuliza.
“Nimekusubiri
wewe unipe ushauri wako. Unajua kwa sasa hivi mimi sina akili kabisa”
“Kwa
sasa hivi huna akili kabisa?” Juma akaniuliza. Kama si ule mkasa wa kusikitisha
ulionipata, bila shaka Juma angeangua kicheko kikali kutokana na jibu langu hilo.
“Kwa
kweli sina akili” Lilikuwa jibu la kipumbavu lakini ulikuwa ndio ukweli
wenyewe.
“Alfred
umefanya kosa moja kubwa!” Juma akaniambia.
“Kosa
gani?”
“Usingeondoka
pale kwa mganga. Ungesubiri zamu yako ya kuingia ukamueleza yule mganga
matatizo yako na kumuonesha yule msichana. Ingekuwa vizuri sana”
“Nilipatwa
na hofu nikajikuta ninaondoka tu”
“Labda
ni yeye aliyekuondoa kimiujiza ili usiingie kwa yule mganga”
“Inawezekana”
“Sasa
inaonekana wewe peke yako hutaweza kujishughulikia. Acha mimi niende Amboni kwa
yule mganga nimueleze matatizo yako”
“Utaenda
sasa hivi?”
“Itabidi
niende sasa hivi”
“Sawa, basi wewe nenda”
Maelezo
yangu pamoja na hali niliyokuwa nayo vilimtia wasiwasi Juma. Akaondoka muda
uleule kwenda Amboni. Mimi nikaendelea kulala. Nilipojihisi kupata nafuu kidogo
nilitoka barazani nikaketi. Ulikuwa ni wakati wa magharibi. Jua lilikuwa
limeshazama likionesha miale ya rangi nyekundu upande wa magharibi.
Sikukaa
sana pale nje
nikarudi ndani kuwasha taa kisha nikabaki mle mle chumbani. Baada ya kupita
karibu saa moja na nusu, Juma akarudi.
“Pole
kwa safari” nikamwambia.
Juma
akaketi kwenye kiti.
“Asante.
Nimekwenda na nimezungumza naye. Nimemueleza kila kitu”
“Amesemaje?”
“Ameshangaa
halafu amecheka. Kilichomchekesha ni wewe kuondoka pale. Amesema ni bora
ungekimbilia kwake, angemkomesha yule jini palepale”
“Sijui
nilifanya upumbavu gani!”
“Sasa
amesema kesho twende asubuhi. Kuna vifaa atavihitaji”
“Kesho
si unaenda kazini?”
“Hapana,
kesho nitakuwa na mapumziko”
“Vifaa
gani ametaka?”
“Ameniambia
nisikutajie hivyo vifaa. Utavikuta huko huko”
“Vina
thamani gani?”
“Kama elfu hamsini hivi”
“Nitakupa”
“Sasa
hivyo vifaa utavinunua wewe?” nikamuuliza Juma.
“Mganga
amesema tumpelekee pesa. Atajua yeye”
“Sawa.
Sasa twende nyumbani nikupe hizo pesa”
“Bado
kuna gharama ya kazi yake”
“Ni
kiasi gani?”
“Hajasema”
“Nina
akiba ya elfu themanini, nitakupa zote”
“Halafu
wewe utabaki na nini?”
“Si
kitu, nataka hili tatizo liishe”
“Hapana,
nipe elfu sitini, bakisha ishirini. Kama
kutahitajika pesa zaidi nitakuongezea mimi”
“Nitakushukuru
sana. Sasa
twende nikakupe hizo elfu sitini”
Tukatoka
mimi na Juma kwenda nyumbani ninakoishi. Tuliingia ndani nikawasha taa na kutoa
shilingi elfu sitini kutoka chini ya godoro, mahali ninakoweka pesa zangu.
Nikampa
Juma zile elfu sitini kisha nikazima taa, tukatoka.
Asubuhi
ya siku iliyofuata tulikwenda kupanda gari tukaenda Amboni. Tulipofika kwa yule
mganga, sisi tulikuwa wa kwanza kwani
tulikuwa tumewahi mapema.
Juma
alipomueleza mganga huyo kuwa mimi ndiye
niliyekwenda kwake jana yake na kuondoka baada ya kumuona yule msichana wa
kijini, mganga aliniambia.
”Hebu
niambie ilikuwaje jana?”
Nikamueleza.
“Ulifanya
kosa kukimbia, ungekuja humu ndani”
“Nilipatwa
na kiwewe mzee”
“Huyo
jini anayekufuata ni Ummi Subiani. Majini hao wana matatizo sana”
“Sasa
mzee nimekuja na zile pesa. Umesema vile vifaa vinagharimu kiasi gani?” Juma
akamuuliza mganga huyo.
“Ni
elfu arubaini”
Juma
akamuhisabia shilingi elfu arubaini na kumpa.
“Vifaa
vyote vinavyohitajika ninavyo hapa. Kazi yenu itafanyika ufukweni mwa bahari.
Itabidi twende huko pamoja na vifaa vyote”
Baada
ya kutuambia hivyo mganga aliwaita wasaidizi wake wawili. Mmoja akamwambia
atangulie na sisi huko ufukweni mwa bahari na mwingine akampa kazi ya
kwenda kuchukua vifaa vilivyohitajika.
Sisi
tukatoka na yule mtu, tukaenda kwa miguu huko ufukweni. Ulikuwa mwendo mrefu
kidogo. Tulipofika hapo mahali, bahari tulikuwa tunaiona mbele yetu. Tukakaa
kwenye mchanga mkavu wa ufukweni kumsubiri mganga.
Mganga
alifika baada ya saa moja hivi akiwa na msiidizi wake wa pili. Mganga mwenyewe
alikuwa ameshika mkuki na kapu lililokuwa na vifaa. Na msaidizi wake alikuwa
ameshika kapu jingine na mkono mwingine alikokota mbuzi mweusi.
ENDELEA
NA HADITHI HII HAPO KESHO UONE KIVUMBI KILICHOTOKEA, Hadithi hii huletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Tiba Cha Mkombozi Sanitarium Clinic Tanga, Mkombozi ni mabingwa wa kutibu magonjwa sugu na hutoa ushauri wa kitaalamu. mkombozi wako na vifaa vya kisasa vya kupima mwili mzima. Mkombozi wamehamia barabara ya 1 Ngamiania Tanga. simu 0654 361333
| |||||||||||||||||
Saturday, April 9, 2016
HADITHI, MWANAMKE ALIENICHUNUKU SEHEMU YA (9)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment