Tangakumekuchablog
Tanga, KAMANDA
wa Polisi Mkoani Tanga, Leonard Poul, ametoa siku 60 kwa wamiliki wa silaha
kuhakiki silaha zao na kuwataka wananchi kutoa taarifa za watu wanaomiliki
silaha kinyume na sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jana, Poul aliwataka wamiliki wa silaha kufanya hivyo kabla ya muda uliowekwa kumalizuika
na kusema kuwa yoyote ambaye hatahakiki atachukuliwa kama mhalifu.
Alisema kufanya hivyo ni kuzuia
matukio ya kihalifu ambayo yamekuwa yakihuisishwa na matumizi ya silaha ambao
kuna baadhi ya watu ambao sio waadilifu silaha zao zimekuwa zikihusishwa.
“Natoa agizo kwa wamiliki wa silaha
Tanga kuhakiki silaha zao kabla ya siku sitini, ambaye hatafa hivyo na silaha
yake kuifungia ndani tutamchukulia kama mhalifu” alisema Poul na kuongeza
“Niwatake wananchi kutoa taarifa kwa
vyombo vya usalama kwa yoyote ambaye anamiliki silaha kinyume na sheria au
kukaidi agizo la uhakiki” alisema
Kamanda aliwataka wananchi
kushirikiana na vyombo vya usalama kuhakikisha kila ambaye anamiliki silaha
anatii agizo hilo ikiwa na pamoja na kuwafichua wamiliki haramu wa silaha.
Aliwataka kila mmoja kwa nafasi yake
na eneo analoishi kutoa ushirikiano wa kuwabaini wamiliki wa silaha na kutoa
taarifa ili kuweza kuwabaini wamiliki haramu wa silaha.
Akizungumzia usalama Mkoani hapa,
Kamanda Poul alisema Mkoa huo uko na usalama na kuwataka wananchi wanaoishi
mpakani mwa Horohoro na Mombasa Kenya kuacha kushirikiana na wafanyabishara wa
magendo.
Alisema kuna baadhi ya watu
wanaoishi mpakani wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara wa magendo hivyo
kuwataka kuacha kufanya hivyo kwani msako wa kuwabaini unaandaliwa.
‘Tunatambua kuwa kuna baadhi ya watu
wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara wa magendo na wapitishaji wa
mihadarati, tunasema tabia hiyo ikomeshwe na dawa yao iko jikoni” alisema
kamanda
Alisema polisi itafanya msako katika
njia za panya ambazo wafanyabiashara wa magendo wamekuwa wakipitishia pamoja na
majumba ambayo huhifadhi hivyo kutoa agizo yoyote ambaye atabainika
atachukuliwa sheria.
Mwisho
No comments:
Post a Comment