Sunday, April 10, 2016

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANGA YATOA TAHADHARI YA KUWEPO MVUA KUBWA



 Mikokoteni na magari yakiwa yameziba barabara ya sita hadi ya tatu Ngamiani Tanga kufuatia mvua kubwa kufunika barabara  ilinyesha jana kuanzia saa tatu asubuhi hadi jioni  leo.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanga (TMA)  imetoa tahadhari kwa wanaoishi mabondeni na wavuvi baharini kuchukua tahadhari kwa madai kuwa mvua ya mara hii itakuwa kubwa na yenye upepo mkali. Mamlaka hiyo pia imewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa familia zao hasa watoto waendapo shule na kurudi kuepuka kupita kandokando ya mifereji mikubwa kwa madai kuwa huweza kutokea mafuriko na maporomoko ya maji kutoka sehemu moja kwenmda kwengine pamoja na milimani.


  Magari na watumiaji wa baskeli wakipita kwa shida barabara ya kwanza Ngamiani Tanga nma baadhi ya nyumba kuingilia na maji ndani kufuatia mvua kubwa iliyonyesha jana kuanzia saa tatu asubuhi hadi jioni leo.

Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment