Mshambuliaji wa Mgambo JKT,
Helbert Chales akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Mbeya City, Haruna
Shamte (28) na Jofrey Mlawa (28) wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara uwanja
wa Mkwakwani leo.
Mshambuliaji wa Mgambo JKT, Helbert Chales, akijaribu kuwatoka wachzaji wa Mbeya City wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani leo.
Mgambo ambao waliuanza mchezo huo kwa kasi na nguvu lakini jitihada zao hazikufua dafu na ilipofika dakika ya 34 Joseph Mahundi aliipatia bao Mbya City.
Hata hivyo kipindi cha pili Mbeya City waliuanza mpira kwa kasi na kuwafunika Mgambo ambapo walikuwa wakilifikia lango la Mbeya City lakini umahiri wa mabeki na Kipa wao Juma Kaseja walinyong'onyea baada ya mipira yao kudakwa.
Hata hivyo Mgambo wanastahili kujilaumu baada ya kupata nafasi mbili za kufunga lakini mashuti yao yalienda fyongo.
No comments:
Post a Comment