Timu ya Mgambo JKT, masaa machache yajayo inatarakiwa kushuka dimbani uwanja wa Mkwakwani kumenyana na timu ya Mbeya City huku kila timu ikitafuta pointi tatu muhimu. Mgambo iliyo na pointi 23 kibindoni itakuwa na kazi ya ziada ya kuibabadua Mbeya City iliyo na Pointi 27 mkononi.
Wachambuzi wa soka wameiambia Tangakumekuchablog kuwa Mgambo haitakubali kuziachia pointi tatu muhimu kwenda Mbeya hivyo ushindi kwao ni wa lazima ikiwa na kuondosha jinamizi la kushuka daraja.
Hata hivyo wachambuzi hao wa mambo ya Kispoti wamesema kuwa Mbeya City hawatabiriki kwani wamekuwa kama Kinyonga kwani hubadilisha mchezo na kutoa matokeo yasiyotarajiwa.
No comments:
Post a Comment