kampuni ya ndege za Airfrance
Ndege hiyo itaanzisha safari zake za ndege mjini Tehran mnamo tarehe 17 mwezi Aprili.
Usimamizi wa kampuni hiyo ulisambaza barua ukiwataka wafanyikazi wake wa kike kuvaa suruali ndefu pamoja na kuvaa vilemba wakati wanapotoka katika ndege hiyo mjin Tehran.
Maafisa wa muungano wa wafanyikazi hao umesema kuwa baadhi ya wafanyikazi wana wasiwasi kuhusu uamuzi huo na wamewataka wakuu wa ndege hiyo kuuondoa uamuzi huo.
Katika mkutano na miungano kadhaa siku ya Jumatatu ,Gilles Gateau,amekiambia kituo cha habari cha Europe 1 kwamba wako tayari kuwepo kwa maelewano.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:
Post a Comment