Tangakumekuchablog
Tanga, WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Ummy Mwalim, Mbunge wa jimbo la Miheza, Adadi Rajab pamoja na Mbunge wa Pangani, Awesoo, leo wanatarajiwa kutembelea eneo la Kibatini kata ya Mzizima Amboni Tanga ambako kulitokea tukio la mauaji ya watu nane kuchinjwa.
vViongozi hao kwa pamoja wanatariwa kutembelea wafiwa na ndugu na jamaa na kujionea kijiji hicho ambacho kwa sasa ni Jangwa baada ya wanakijiji wote kuhama makazi yao.
Usiku wa Jumatatu watu 8 walikusanywa nje ya uwanja wa nyumba ya Mwenyekiti wa kitongoji na kuchinjwa mmoja baada ya mmoja kisha kutokomea kusikojulikana.
Tukio hilo ambalo linadaiwa kufanywa na Majambazi kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Tanga, Leonard Poul limefanyika huku kukiwa na matukio mfululizo.
Mkuu wa Majeshi nchini, Devid Mamunyange, IGP, Enerst Magu, Naibu Waziri wa mambo ya ndani, Hamadi Masauni walifika katika eneo la tukio na kutoa agizo kali la kutaka watu waliofanya kitendo hicho wamakatwe haraka na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Fuatilia blog hii kwa picha na yote yatakayojiri huko
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment