Ikifika saa moja kama wewe ni mtu mweusi huruhusiwi kuingia Mgahawa huu Nairobi !!
Kumekuwa na story nyingi toka Kenya
kuhusiana na matukio ya uvamizi na mauaji ambayo yanahusishwa na Kikundi
cha kigaidi cha Al Shabaab.. Watu wengi wanahofia usalama wao hasa
maeneo ambayo yana mkusanyiko mkubwa wa watu.
Mgahawa mmoja unaomilikiwa na watu wenye
asili ya China maeneo ya Kilimani, Nairobi Kenya umeingia kwenye
Headlines kutokana na sheria waliyoweka ya kuwazuia wakenya na mtu
yoyote ambaye ni mweusi kungia kwenye mgahawa huo baada ya saa 11 jioni.
Mgahawa huo umeweka sheria hiyo kali
kutokana na tukio la uvamizi lililotokea mwaka jana, kwa madai kuwa
genge la majambazi waliingia katika mgahawa huo wakijifanya kuwa ni
wateja, baadaye wakawateka na kuwapora wateja pamoja na pesa zote za
mauzo ya mgahawani hapo.
Kwa upande wa Afisa wa masuala ya raia nchini humo, Otiende Amollo amesema
sheria hiyo ni kinyume cha sheria, inakiuka uhuru wa wakenya na
inawafanya watu weusi kuonekana kuwa ni majambazi na kuitaka tume ya
kupigania haki za kibinadamu kuushtaki mgahawa huo kwa kukiuka maadili.
Msemaji wa Mgahawa huo amesema waafrika
wachache wanaruhusiwa kwa sababu ni waaminifu na wateja wao wamefurahia
sheria hiyo kali ambayo wanaona inawahakikishia usalama wao kwa sababu
ni vigumu kugundua watu wanaojihusisha na kundi la Al Shabaab iwapo
wakiingia kama wateja.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment