Kisa cha Polisi kususiwa maiti safari hii ni Kenya mtu wangu..
Katika kaunti ya Nyeri nchini Kenya kuna
tukio lililotokea juzi March 26 ambapo watu waliokuwa wakiomboleza
walichukua mwili wa mtu mmoja na kwenda nao katika kituo cha Polisi cha Mkurueni wakidai Polisi walihusika na kifo cha mtu huyo.
Waombolezaji hao walichukua mwili huo
katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Nyeri na kuandamana hadi
kituo hicho kwa madai mwanaume huyo alipigwa risasi na Polisi wa kituo
hicho, walikutana na maafisa wa Polisi ambao walijaribu kuwazuia lakini
waliwashinda nguvu na kuweka jeneza kwenye mlango wa kituo hicho na
kuondoka.
Polisi waliwarushia mabomu ya machozi
ili kuwatawanya, baadaye walikubaliana hali ikakaa sawa ambapo ndugu wa
marehemu huyo walikubali kuuchukua mwili na kwenda kufanya mazishi.
No comments:
Post a Comment