Maamuzi mapya ya Australia baada ya kujulikana Rubani aliiangusha ndege ya Ujerumani kwa makusudi
Truss amesema mashirika ya ndege ya
Australia ikiwemo Qantas na Virgin Australia wameanza kuyafanyia kazi
mabadiliko ya usalama ambapo kuanzia sasa hakuna cha Rubani kubaki
mwenyewe kwenye chumba cha Marubani, kama wako wawili na mmoja akawa
anataka kutoka labda kwenda Toilet, inabidi muhudumu mmoja wa ndege
aingie kwenye chumba hicho ndio rubani mmoja atoke.
Mabadiliko haya yameanza kufanyiwa kazi
toka Jumatatu mchana March 30 2015 ambapo mwanzoni ilikua inaruhusiwa
kwa Rubani mmoja kupaki kwenye chumba cha kurushia ndege.
Hii yote imekuja baada ya Rubani msaidizi
kwenye ndege ya Ujerumani iliyoanguka Ufaransa kugundulika kwamba
aliiangusha ndege kwa makusudi na ni baada ya Rubani mkuu kutoka nje ya
chumba cha Marubani, alipotaka kurudi akakuta mlango umefungwa, yaani
rubani msaidizi ndio kajifungia na akaiangusha ndege kwa makusudi.
No comments:
Post a Comment