Huwa unadata na nyumba nzuri nzuri? leo nimedata na hizi.
Ujenzi wa nyumba nzima kama hizi unaweza
kuwa kikwazo kwako sababu ya kipato lakini mimi na wewe tunaweza kupata
idea hata chache za kuhamishia kwenye nyumba za uwezo wetu na bado
tukawa washindi.
Siku
hizi bongo naona watu wengi wanakwepa rangi nyeupe na kuweka blue au
kijani, labda huyu mwenye hii nyumba ameweza kubadilisha mtazamo wetu
Hii nyumba ya pili ni kwa wale watu wangu wanaopenda kuwa na nafasi kubwa nyumbani.
Hii sebule imenivutia jinsi walivyo tumia ubunifu kuweka kochi moja badala ya kuweka matatu ambapo pasingetosha.
Hakuna
haja ya kuwa na kabati la TV ndio uonekane wa kisasa, uwekaji wa TV
kwenye ukuta ndio wa kisasa zaidi au kuwa na kabati dogo kama hili.
Umependa nini ulichokiona kwenye hizi za leo mtu wangu?
No comments:
Post a Comment