Yako mengi Duniani, na hii simu iliyotengenezwa kwa majani umeipata?
Teknolojia inatufungulia mapya kila
siku.. Nakumbuka simu za kwanza za mkononi zilikuwa kubwa halafu nzito,
baadae ikaja fashion ya simu ndogo ndogo, zile kubwa watu wakawa
wanaziita ‘mshindi’ ambalo ni jina la sabuni… Sasa hivi tunaona fashion
ya simu kubwa inarudi mdogomdogo.
Sean Miles anaingia
kwenye historia, anaingia kwenye headlines pia.. yeye kagundua hii simu
ambayo imetengenezwa kwa majani kabisa pamoja na mchanganyiko wa vitu
vingine vilivyochakaa ama vilivyoharibika.
Unaambiwa cover ya simu hii ukiiangalia ni kama majani kabisa.
Vipi mtu wangu ukikutana na hii simu pale Ngamiani au Mitaa ya Posta pale Market Street? kuna kitu kitakufanya usiipende labda?
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment