
Baada ya watu kuhoji ishu ya kampuni ya
Kidoti kutengeneza ndala ambazo ni maalum kwa wanawake na kuonekama kama amewasahau wanaume,
Jokate
ambae amesema kutakuwa na brand maalum ya wanaume na wataanza kuzipata
muda wowote, akizungumzia kuhusu bei kuwa juu amesema watu wanaochukua
ndio wanapandisha bei kutokana na gharama za kwenda kuchukua.

Mwanamziki
Vee Money wiki hii anategemea kuachia ngoma mpya aliyomshirikisha Rapa kutoka Afrika Kusini
KO,
akizungumzia ngoma hiyo amesema ni wimbo unayohusu mapenzi ya dhati
ambao ni maalum kwa watu wote wanaopendana, kuhusu kumshirikisha
KO
amesema alikuwa anatamani kufanyanae kazi kwa muda mrefu lakini hakuwa
na uhakika kama atapata ushirikiano lakini aliweza kuzungumza nae na
kufanikiwa kufanya nae kazi.

Muigizaji
Wema Sepetu
amesema mitandao ya kijamii inanafasi kubwa katika maisha yake hasa
katika maswala ya utangazaji na kutolea mfano mtandao wa Istagaram na
kusema, umerahisisha kazi kutokana na kutumiwa sana katika matangazo,
yeye ameweza kujua maduka mengi na vitu vingi kupitia mtandao huo na
endapo mtu akitaka apost kazi yake kwenye page yake ni kama dola elfu
moja au elfu mbili lakini inategemea na makubaliano.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment