Ubunifu mwingine kwenye mijengo mtu wangu.. Nimevutiwa sana na hizi PICHAZ
Nyumba za vioo, nyumba za miti.. Ziko nyingi hapa , unaweza kuzicheki zote.
Trojan Horse Hotel.
Kwa haraka haraka unaweza usijue hiki ni nini, lakini unaambiwa hii ni
Hotel, hapo ndani kuna vyumba vya kulala na kila kitu kinaenda poa
kabisa.
Ark Hotel, China.
Wachina na teknolojia zao mtu wangu, hii Hotel imetengenezwa kwenye
maji inaelea yani. Hapo unaweza kuona kwa juu inavyoonekana na kwa ndani
ya maji pia.
Mirror Tree House, Sweden.
Hapo panapoonekana kama mwanga mwekundu ni chumba cha Hotel yani,
kimejengwa kwa vioo vitupu. Utakuwa na amani kweli kulala hapo?
Unadhani hii ni karavati ya barabarani? Hapana.. Ni vyumba vya Das Park Hotel, iko Austria. Vyumba nd’o viko hivyo yani. Mambo ya Ulaya Ulaya.
Bubble Hotel, unaweza kujionea hiii mtu wangu ukitembelea Ufaransa.
Moja ya story zilizosikika March 2015 ni malalamiko ya baadhi ya watu
kwamba hakuna usiri wowote ukiwa ndani ya chumba hicho cha Hotel.
No comments:
Post a Comment