Van Gaal na tuzo maalum ya heshima kutoka Uholanzi.
Pamoja na kutokuwa na kiwango kizuri lakini bosi wa klabu hiyo Louis Van Gaal ameweza kuibuka mshindi katika tuzo maarufu ya Anton Geesink ambayo hutolewa nchini Uholanzi.
Tuzo hiyo maalum hutolewa kwa mtu, mji au kundi la watu lililofanya vema katika michezo mbalimbali.
Van Gaal ambaye kikosi chake cha Man
united hakiko katika kiwango kizuri msimu huu amepewa tuzo hiyo baada ya
Uholanzi kuonyesha kiwango bora na kushika nafasi ya tatu katika Kombe
la Dunia nchini Brazil, mwaka jana.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment