Rais Kagame kuhusu Tanzania na Rwanda, saa kadhaa baada ya Rais Magufuli kurudi Tanzania
Kwenye nukuu zilizotolewa na ofisi ya Rais Rwanda kutoka kwa Rais Kagame ambaye aliyasema haya baada ya Rais Magufuli kuondoka Rwanda, ni pamoja na hii >>> ‘Kwa uongozi mpya, sasa Rwanda na Tanzania watafurahia uhusiano mzuri na kila tatizo litatuliwa‘
Hii ni kauli ambayo Rais Kagame aliisema wakati wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari Rwanda na aliyazungumza haya mbele ya maelfu ya Wananchi waliokusanyika kwenye uwanja wa mpira Amahoro Kigali Rwanda ambapo pia Rais Kagame alimshukuru Rais Magufuli kwa kuitembelea Rwanda kupitia page yake ya Twitter.
Rais Kagame alisisitiza pia kwamba ‘Wote wanaojaribu kuliangamiza taifa letu ikiwemo na wale wanaowatumia nchi ambazo ni jirani zetu kamwe hawatoweza kufanikiwa‘
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment