Mwembe uliopo Tangamano Tanga
ukiwa katika muonekano kama wa sura ya Muasisi wa Taifa, Mwalimu Nyerere na
kuwa kivutio kwa wakazi wa jiji hilo pamoja na Wilaya za jirani ikiwemo Pangani, Mkinga na Muheza.
Mwembe huo ambao upo kwa miaka mingi ulipo uwanja maarufu wa mikutano wa Tangamano, muembe huo ulikuwa bado haujagundulika na juzi usiku watu wamedai kuona maajabu ya kuwaka taa na kuonekana sura ilioyofanana na Muasisi wa Taifa hili.
Taarifa zilianza kusambaa na watu kumiminika usiku mchana kujionea maajabu hayo jambo ambalo hata viongozi wakuu wa Idara na Serikali ni miongoni mwa watu walienda kujinea maajabu hayo.
Maelfu ya wakazi wa Tanga na viunga vyake wanamiminika kujionea, hata hivyo baadhi ya watu wameiambia tangakumekuchablog kuwa maajabu hayo yanaweza kuwa moja ya vivutio vya Utalii Tanga
No comments:
Post a Comment