Kampuni ya kuzalisha umeme nchini
Kenya, KENGEN imetuma taarifa kwa vyombo vya habari ikiomba radhi kwa
ukosefu wa umeme jana.
Mara kwa mara umeme hupotea nchini Kenya kwa sababu moja au nyengine, sawa tu na mataifa yote barani AfrikaHata hivyo sababu walioitoa KENGEN kwa ukosefu huo wa umeme Kwa takriban saa nne kote nchini humo ndio imewaacha wengi wamepigwa na butwaa !
Amini usiamini, KENGEN imempata nyani mmoja katika eneo maalum lenye 'swichi' hiyo katika mtambo wa kuzalisha umeme ulioko kwenye bwawa kuu la Gitaru Mashariki mwa Kenya.
Sasa kampuni hiyo inasema huenda nyani huyo ndiye aliyezima umeme kote nchini Kenya !
Kengen inasema kuwa huenda nyani huyo aliangukia mashine hiyo ndogo na ''kusababisha hitilafu ya takriban megawati 180 za umeme ambao ndio uliosababisha ukosefu wa umeme kote nchini Kenya.''
Kwa takriban saa nne taarifa hiyo ilielezea.
BBC
No comments:
Post a Comment